Mwanzo 8:7
Genesis 8:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
na akamtoa kunguru, akawa akiruka kwenda na kurudi mpaka maji yalipokwisha kukauka juu ya nchi.
Genesis 8:7 in English
Genesis 8:7 · Berean Standard Bible
and sent out a raven. It kept flying back and forth until the waters had dried up from the earth.
Context
5Maji yakaendelea kupungua hadi mwezi wa kumi, na siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima vikaonekana. 6Baada ya siku arobaini Noa akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina 7na akamtoa kunguru, akawa akiruka kwenda na kurudi mpaka maji yalipokwisha kukauka juu ya nchi. 8Kisha akamtoa hua ili aone kama maji yameondoka juu ya uso wa ardhi. 9Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Noa ndani ya safina. Noa akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.