Mwanzo 8:2
Genesis 8:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Zile chemchemi zilizo chini sana ya ardhi pamoja na malango ya mafuriko ya mbinguni yakawa yamefungwa nayo mvua ikawa imekoma kunyesha kutoka angani.
Genesis 8:2 in English
Genesis 8:2 · Berean Standard Bible
The springs of the deep and the floodgates of the heavens were closed, and the rain from the sky was restrained.
Context
1Mungu akamkumbuka Noa na wanyama wote wa porini na wa kufugwa waliokuwa naye ndani ya safina, akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakaondoka. 2Zile chemchemi zilizo chini sana ya ardhi pamoja na malango ya mafuriko ya mbinguni yakawa yamefungwa nayo mvua ikawa imekoma kunyesha kutoka angani. 3Maji yakaendelea kupungua taratibu katika nchi. Kunako mwisho wa siku ya 150, maji yalikuwa yamepungua, 4katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa saba, safina ikatua katika milima ya Ararati.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.