Native Bible

Genesis 8:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Noa akangojea siku saba zaidi kisha akamtoa tena hua kutoka safina.

Genesis 8:10 in English

Genesis 8:10 · Berean Standard Bible

Noah waited seven more days and again sent out the dove from the ark.

Context

8Kisha akamtoa hua ili aone kama maji yameondoka juu ya uso wa ardhi. 9Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Noa ndani ya safina. Noa akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina. 10Noa akangojea siku saba zaidi kisha akamtoa tena hua kutoka safina. 11Wakati hua aliporejea kwa Noa jioni, alikuwa amechukua katika mdomo wake jani bichi la mzeituni, lililochumwa wakati ule ule! Ndipo Noa akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya uso wa dunia. 12Akangojea siku saba zaidi na akamtuma tena hua, lakini wakati huu hua hakurudi tena kwa Noa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.