Native Bible

Genesis 42:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ingawa Yosefu aliwatambua ndugu zake, wao hawakumtambua.

Genesis 42:8 in English

Genesis 42:8 · Berean Standard Bible

Although Joseph recognized his brothers, they did not recognize him.

Context

6Wakati huo Yosefu alikuwa mtawala wa nchi ya Misri, naye alikuwa ndiye aliwauzia watu wote nafaka. Kwa hiyo wakati ndugu zake Yosefu walipofika, wakamsujudia hadi nyuso zao zikagusa ardhi. 7Mara Yosefu alipowaona ndugu zake, akawatambua, lakini akajifanya mgeni na kuzungumza nao kwa ukali, akiwauliza, “Ninyi mnatoka wapi?” Wakamjibu, “Tumetoka katika nchi ya Kanaani kuja kununua chakula.” 8Ingawa Yosefu aliwatambua ndugu zake, wao hawakumtambua. 9Ndipo Yosefu alipokumbuka ndoto zake kuwahusu wao, akawaambia, “Ninyi ni wapelelezi! Mmekuja kuangalia mahali ambapo nchi yetu haina ulinzi.” 10Wakamjibu, “Sivyo bwana wangu. Watumishi wako wamekuja kununua chakula.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.