Mwanzo 42:3
Genesis 42:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo wale ndugu kumi wa Yosefu, wakateremka huko Misri kununua nafaka.
Genesis 42:3 in English
Genesis 42:3 · Berean Standard Bible
So ten of Joseph’s brothers went down to buy grain from Egypt.
Context
1Wakati Yakobo alipofahamu kuwa kuna nafaka huko Misri, akawaambia wanawe, “Mbona mnakaa tu hapa mnatazamana?” 2Akaendelea kuwaambia, “Nimesikia kuwa huko Misri kuna nafaka. Telemkeni huko mkanunue chakula kwa ajili yetu, ili tuweze kuishi wala tusife.” 3Ndipo wale ndugu kumi wa Yosefu, wakateremka huko Misri kununua nafaka. 4Lakini Yakobo hakumtuma Benyamini, ndugu yake Yosefu, pamoja na wengine, kwa sababu aliogopa asije akapatwa na madhara. 5Hivyo wana wa Israeli walikuwa miongoni mwa wale waliokwenda Misri kununua nafaka, kwani njaa ilikuwa katika nchi ya Kanaani pia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.