Native Bible

Genesis 42:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yosefu akatoa amri ya kujaza magunia yao nafaka na kuweka fedha ya kila mmoja ndani ya gunia lake, kisha wapewe mahitaji ya njiani. Baada ya kufanyiwa hayo yote,

Genesis 42:25 in English

Genesis 42:25 · Berean Standard Bible

Then Joseph gave orders to fill their bags with grain, to return each man’s silver * to his sack, and to give them provisions for their journey. This order was carried out,

Context

23Hawakujua kuwa Yosefu angewaelewa, kwa sababu alitumia mkalimani. 24Yosefu akajitenga nao akaanza kulia, kisha akawarudia na kuzungumza nao tena. Akataka Simeoni akamatwe na kufungwa mbele yao. 25Yosefu akatoa amri ya kujaza magunia yao nafaka na kuweka fedha ya kila mmoja ndani ya gunia lake, kisha wapewe mahitaji ya njiani. Baada ya kufanyiwa hayo yote, 26wakapakiza nafaka juu ya punda zao, wakaondoka. 27Walipofika mahali pa kulala huko njiani mmoja wao akafungua gunia lake ili amlishe punda wake, akakuta fedha yake kwenye mdomo wa gunia lake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.