Mwanzo 42:23
Genesis 42:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hawakujua kuwa Yosefu angewaelewa, kwa sababu alitumia mkalimani.
Genesis 42:23 in English
Genesis 42:23 · Berean Standard Bible
They did not realize that Joseph understood them, since there was an interpreter between them.
Context
21Wakaambiana wao kwa wao, “Hakika tunaadhibiwa kwa sababu ya ndugu yetu. Tuliona jinsi alivyohuzunika alipokuwa anatusihi kuponya maisha yake, lakini hatukumsikiliza, hiyo ndiyo sababu dhiki hii imetupata.” 22Reubeni akawajibu, “Sikuwaambieni msitende dhambi dhidi ya kijana? Lakini hamkunisikiliza! Sasa ni lazima tuadhibiwe kwa ajili ya damu yake.” 23Hawakujua kuwa Yosefu angewaelewa, kwa sababu alitumia mkalimani. 24Yosefu akajitenga nao akaanza kulia, kisha akawarudia na kuzungumza nao tena. Akataka Simeoni akamatwe na kufungwa mbele yao. 25Yosefu akatoa amri ya kujaza magunia yao nafaka na kuweka fedha ya kila mmoja ndani ya gunia lake, kisha wapewe mahitaji ya njiani. Baada ya kufanyiwa hayo yote,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.