Mwanzo 40:3
Genesis 40:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
akawaweka chini ya ulinzi katika nyumba ya mkuu wa kikosi cha ulinzi katika gereza lile lile alimofungwa Yosefu.
Genesis 40:3 in English
Genesis 40:3 · Berean Standard Bible
and imprisoned them in the house of the captain of the guard, the same prison where Joseph was confined.
Context
1Baada ya muda, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri. 2Farao akawakasirikia hawa maafisa wake wawili, mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, 3akawaweka chini ya ulinzi katika nyumba ya mkuu wa kikosi cha ulinzi katika gereza lile lile alimofungwa Yosefu. 4Mkuu wa kikosi cha ulinzi akawakabidhi kwa Yosefu, naye akawahudumia.
Walipokuwa wamekaa chini ya ulinzi kwa muda, 5kila mmoja wa hao wawili waliokuwa wamewekwa gerezani, yaani mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, waliota ndoto usiku mmoja, na kila ndoto ilikuwa na maana yake tofauti.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.