Mwanzo 4:3
Genesis 4:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwa Bwana.
Genesis 4:3 in English
Genesis 4:3 · Berean Standard Bible
So in the course of time, Cain brought some of the fruit of the soil as an offering to the LORD,
Context
1Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada wa Bwana nimemzaa mwanaume.” 2Baadaye akamzaa Abeli ndugu yake.
Basi Abeli akawa mfugaji, na Kaini akawa mkulima. 3Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwa Bwana. 4Lakini Abeli akaleta fungu nono kutoka baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. Bwana akamkubali Abeli pamoja na sadaka yake, 5lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.