Mwanzo 4:19
Genesis 4:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila.
Genesis 4:19 in English
Genesis 4:19 · Berean Standard Bible
And Lamech married two women, one named Adah and the other Zillah.
Context
17Kaini akakutana kimwili na mkewe, naye akapata mimba na akamzaa Enoki. Wakati huo Kaini alikuwa anajenga mji, akauita Enoki jina la mtoto wake. 18Enoki akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli, Mehuyaeli akamzaa Methushaeli, na Methushaeli akamzaa Lameki. 19Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila. 20Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama. 21Kaka yake aliitwa Yubali, aliyekuwa baba wa wote wapigao zeze na filimbi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.