Mwanzo 39:16
Genesis 39:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yule mwanamke akaliweka lile vazi karibu naye mpaka Potifa aliporudi nyumbani.
Genesis 39:16 in English
Genesis 39:16 · Berean Standard Bible
So Potiphar’s wife kept Joseph’s cloak beside her until his master came home.
Context
14akawaita watumishi wake wa nyumbani, akawaambia, “Tazameni! Huyu Mwebrania ameletwa hapa kutudhihaki! Aliingia hapa ndani ili akutane nami kimwili, lakini nikapiga kelele. 15Aliposikia kelele za kuomba msaada, akaacha vazi lake kando yangu akakimbilia nje.” 16Yule mwanamke akaliweka lile vazi karibu naye mpaka Potifa aliporudi nyumbani. 17Ndipo akamweleza kisa hiki, akisema: “Yule mtumwa wa Kiebrania uliyetuletea alinijia ili kunidhihaki. 18Lakini mara nilipopiga kelele kuomba msaada, akaliacha vazi lake kando yangu akakimbia nje ya nyumba.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.