Mwanzo 35:20
Genesis 35:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Juu ya kaburi lake, Yakobo akasimamisha nguzo, ambayo mpaka leo inatambulisha kaburi la Raheli.
Genesis 35:20 in English
Genesis 35:20 · Berean Standard Bible
Jacob set up a pillar on her grave; it marks Rachel’s tomb to this day.
Context
18Hapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe Benoni.* Lakini babaye akamwita Benyamini.* 19Kwa hiyo Raheli akafa, akazikwa kando ya njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). 20Juu ya kaburi lake, Yakobo akasimamisha nguzo, ambayo mpaka leo inatambulisha kaburi la Raheli. 21Israeli akaendelea tena na safari yake na kupiga hema mbele mnara wa Ederi. 22Wakati Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aitwaye Bilha, naye Israeli akasikia jambo hili.
Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.