Native Bible

Genesis 35:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Alipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.”

Genesis 35:17 in English

Genesis 35:17 · Berean Standard Bible

During her severe labor, the midwife said to her, “Do not be afraid, for you are having another son.”

Context

15Yakobo akapaita mahali pale Mungu alipozungumza naye Betheli.* 16Kisha wakaondoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efrathi, Raheli akaanza kusikia uchungu na alipata shida kuu. 17Alipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.” 18Hapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe Benoni.* Lakini babaye akamwita Benyamini.* 19Kwa hiyo Raheli akafa, akazikwa kando ya njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu).

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.