Native Bible

Genesis 35:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.”

Genesis 35:12 in English

Genesis 35:12 · Berean Standard Bible

The land that I gave to Abraham and Isaac I will give to you, and I will give this land to your descendants after you.”

Context

10Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo, lakini hutaitwa tena Yakobo, jina lako utakuwa Israeli.” Kwa hiyo akamwita Israeli. 11Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi,* ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako. 12Nchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.” 13Kisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye. 14Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.