Native Bible

Genesis 35:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi,* ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako.

Genesis 35:11 in English

Genesis 35:11 · Berean Standard Bible

And God told him, “I am God Almighty.* Be fruitful and multiply. A nation—even a company of nations—shall come from you, and kings shall descend from you.

Context

9Baada ya Yakobo kurudi kutoka Padan-Aramu, Mungu alimtokea tena na kumbariki. 10Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo, lakini hutaitwa tena Yakobo, jina lako utakuwa Israeli.” Kwa hiyo akamwita Israeli. 11Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi,* ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako. 12Nchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.” 13Kisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.