Mwanzo 34:4
Genesis 34:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Shekemu akamwambia baba yake Hamori, “Nipatie msichana huyu awe mke wangu.”
Genesis 34:4 in English
Genesis 34:4 · Berean Standard Bible
So Shechem told his father Hamor, “Get me this girl as a wife.”
Context
2Ikawa Shekemu mwana wa Hamori Mhivi, mtawala wa eneo lile alipomwona, akamchukua na kumnajisi. 3Moyo wake ukavutwa sana kwa Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana na akazungumza naye kwa kumbembeleza. 4Shekemu akamwambia baba yake Hamori, “Nipatie msichana huyu awe mke wangu.” 5Yakobo aliposikia kwamba binti yake Dina amenajisiwa, wanawe walikuwa mashambani wakichunga mifugo yake, kwa hiyo akalinyamazia jambo hilo mpaka waliporudi nyumbani. 6Kisha Hamori baba yake Shekemu akaenda kuzungumza na Yakobo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.