Mwanzo 33:7
Genesis 33:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Lea na watoto wake wakaja na kusujudu. Mwisho wa wote wakaja Yosefu na Raheli, nao pia wakasujudu.
Genesis 33:7 in English
Genesis 33:7 · Berean Standard Bible
Leah and her children also approached and bowed down, and then Joseph and Rachel approached and bowed down.
Context
5Esau akainua macho akawaona wale wanawake na watoto. Akauliza, “Hawa uliofuatana nao ni nani?”
Yakobo akamjibu, “Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema.” 6Kisha wale watumishi wa kike na watoto wao wakakaribia na kusujudu. 7Kisha Lea na watoto wake wakaja na kusujudu. Mwisho wa wote wakaja Yosefu na Raheli, nao pia wakasujudu. 8Esau akauliza, “Una maana gani kuhusu makundi hayo yote niliyokutana nayo?”
Akasema, “Ni ili kupata kibali machoni pako, bwana wangu.” 9Lakini Esau akamwambia, “Ndugu yangu, tayari nina wingi wa mali. Ulivyo navyo viwe vyako mwenyewe.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.