Mwanzo 32:30
Genesis 32:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo Yakobo akapaita mahali pale Penieli,* akasema, “Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso na bado maisha yangu yameokoka.”
Genesis 32:30 in English
Genesis 32:30 · Berean Standard Bible
So Jacob named the place Peniel,* saying, “Indeed, I have seen God face to face, and yet my life was spared.”
Context
28Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli,* kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.” 29Yakobo akasema, “Tafadhali niambie jina lako.”
Lakini akajibu, “Kwa nini kuniuliza Jina langu?” Ndipo akambariki huko. 30Kwa hiyo Yakobo akapaita mahali pale Penieli,* akasema, “Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso na bado maisha yangu yameokoka.” 31Jua lilikuwa linachomoza Yakobo alipoondoka Penueli, naye alikuwa akichechemea kwa sababu ya nyonga yake. 32Kwa hiyo mpaka leo Waisraeli hawali mshipa ulioungana na kiungio cha nyonga, kwa sababu kiungio cha nyonga ya Yakobo kiliteguliwa karibu na mshipa huo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.