Mwanzo 31:23
Genesis 31:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akiwachukua jamaa zake, akamfuatia Yakobo kwa siku saba na kumkuta kwenye nchi ya vilima katika Gileadi.
Genesis 31:23 in English
Genesis 31:23 · Berean Standard Bible
So he took his relatives with him, pursued Jacob for seven days, and overtook him in the hill country of Gilead.
Context
21Hivyo akakimbia pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo na kuvuka Mto Frati akaelekea nchi ya vilima katika Gileadi. 22Siku ya tatu Labani akaambiwa kwamba Yakobo amekimbia. 23Akiwachukua jamaa zake, akamfuatia Yakobo kwa siku saba na kumkuta kwenye nchi ya vilima katika Gileadi. 24Ndipo Mungu akamjia Labani Mwaramu katika ndoto usiku na kumwambia, “Jihadhari usiseme neno lolote kwa Yakobo, liwe zuri au baya.” 25Yakobo alikuwa amepiga hema lake katika nchi ya vilima katika Gileadi wakati Labani alipomkuta, Labani na jamaa yake wakapiga kambi huko pia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.