Native Bible

Genesis 31:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Labani alipokuwa amekwenda kukata kondoo wake manyoya, Raheli aliiba miungu ya nyumba ya baba yake.

Genesis 31:19 in English

Genesis 31:19 · Berean Standard Bible

Now while Laban was out shearing his sheep, Rachel stole her father’s household idols.

Context

17Ndipo Yakobo akawapandisha watoto wake na wake zake juu ya ngamia, 18naye akawaswaga wanyama wote mbele yake pamoja na vitu vyote alivyokuwa amechuma huko Padan-Aramu kwenda kwa baba yake Isaki katika nchi ya Kanaani. 19Labani alipokuwa amekwenda kukata kondoo wake manyoya, Raheli aliiba miungu ya nyumba ya baba yake. 20Zaidi ya hayo, Yakobo alimdanganya Labani Mwaramu kwa kutokumwambia kwamba anakimbia. 21Hivyo akakimbia pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo na kuvuka Mto Frati akaelekea nchi ya vilima katika Gileadi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.