Mwanzo 30:8
Genesis 30:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Raheli akasema, “Nilikuwa na mashindano makubwa na ndugu yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita Naftali.*
Genesis 30:8 in English
Genesis 30:8 · Berean Standard Bible
Then Rachel said, “In my great struggles, I have wrestled with my sister and won.” So she named him Naphtali.*
Context
6Ndipo Raheli akasema, “Mungu amenipa haki yangu, amesikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita Dani.* 7Bilha mtumishi wa kike wa Raheli akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. 8Ndipo Raheli akasema, “Nilikuwa na mashindano makubwa na ndugu yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita Naftali.* 9Lea alipoona kuwa amekoma kuzaa watoto, alimchukua mtumishi wake wa kike Zilpa, naye akampa Yakobo awe mke wake. 10Mtumishi wa Lea yaani Zilpa, akamzalia Yakobo mwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.