Native Bible

Genesis 30:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo Raheli akasema, “Mungu amenipa haki yangu, amesikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita Dani.*

Genesis 30:6 in English

Genesis 30:6 · Berean Standard Bible

Then Rachel said, “God has vindicated me; He has heard my plea and given me a son.” So she named him Dan.*

Context

4Hivyo Raheli akampa Yakobo Bilha awe mke wake. Yakobo akakutana naye kimwili, 5Bilha akapata mimba, naye akamzalia Yakobo mwana. 6Ndipo Raheli akasema, “Mungu amenipa haki yangu, amesikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita Dani.* 7Bilha mtumishi wa kike wa Raheli akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. 8Ndipo Raheli akasema, “Nilikuwa na mashindano makubwa na ndugu yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita Naftali.*

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.