Mwanzo 3:4
Genesis 3:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa.
Genesis 3:4 in English
Genesis 3:4 · Berean Standard Bible
“You will not surely die,” the serpent told her.
Context
2Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini, 3lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ” 4Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa. 5Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” 6Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.