Native Bible

Genesis 28:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake naye amekwenda Padan-Aramu.

Genesis 28:7 in English

Genesis 28:7 · Berean Standard Bible

and that Jacob had obeyed his father and mother and gone to Paddan-aram.

Context

5Kisha Isaki akamuaga Yakobo, naye akaenda Padan-Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, ndugu wa Rebeka, aliyekuwa mama wa Yakobo na Esau. 6Sasa Esau akajua kuwa Isaki amembariki Yakobo na kumtuma kwenda Padan-Aramu ili achukue mke huko na kwamba alipombariki alimwamuru akisema, “Usioe mke katika binti za Wakanaani,” 7tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake naye amekwenda Padan-Aramu. 8Esau akatambua jinsi ambavyo baba yake Isaki anavyowachukia binti za Wakanaani. 9Ndipo Esau akaenda kwa Ishmaeli, akamwoa Mahalati, ndugu wa Nebayothi na binti wa Ishmaeli mwana wa Abrahamu, kuongezea wale wake wengine aliokuwa nao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.