Mwanzo 27:26
Genesis 27:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Isaki baba yake akamwambia, “Njoo hapa, mwanangu, unibusu.”
Genesis 27:26 in English
Genesis 27:26 · Berean Standard Bible
Then his father Isaac said to him, “Please come near and kiss me, my son.”
Context
24Akamuuliza, “Hivi kweli wewe ni mwanangu Esau?”
Akajibu, “Mimi ndiye.” 25Kisha akasema, “Mwanangu, niletee sehemu ya mawindo yako nile, ili nipate kukubariki.”
Yakobo akamletea naye akala, akamletea na divai akanywa. 26Kisha Isaki baba yake akamwambia, “Njoo hapa, mwanangu, unibusu.” 27Kwa hiyo akamwendea akambusu. Isaki aliposikia harufu ya nguo zake, akambariki, akasema,
“Aha, harufu ya mwanangu
ni kama harufu ya shamba
ambalo Bwana amelibariki. 28Mungu na akupe umande kutoka mbinguni
na utajiri wa duniani:
wingi wa nafaka na divai mpya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.