Native Bible

Genesis 25:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yakobo akamjibu, “Niuzie kwanza haki yako ya mzaliwa wa kwanza.”

Genesis 25:31 in English

Genesis 25:31 · Berean Standard Bible

“First sell me your birthright,” Jacob replied.

Context

29Siku moja Yakobo alipika mchuzi wa dengu, Esau akarudi kutoka porini akiwa na njaa kali. 30Esau akamwambia Yakobo, “Haraka, nipe huo mchuzi mwekundu! Nina njaa kali sana!” (Hii ndiyo sababu pia aliitwa Edomu.)* 31Yakobo akamjibu, “Niuzie kwanza haki yako ya mzaliwa wa kwanza.” 32Esau akasema, “Tazama, mimi niko karibu ya kufa, itanifaa nini haki ya mzaliwa wa kwanza?” 33Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Hivyo Esau akamwapia, akamuuzia Yakobo haki yake ya kuzaliwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.