Mwanzo 24:22
Genesis 24:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ikawa ngamia walipokwisha kunywa wote, yule mtumishi akampa huyo msichana pete ya puani ya dhahabu yenye uzito wa beka moja* na bangili mbili za dhahabu zenye uzito wa shekeli kumi.*
Genesis 24:22 in English
Genesis 24:22 · Berean Standard Bible
And after the camels had finished drinking, he took out a gold ring weighing a beka,* and two gold bracelets for her wrists weighing ten shekels.*
Context
20Akafanya haraka kumimina maji kwenye birika ya kunyweshea wanyama, akakimbia kisimani kuteka maji mengine na akateka ya kuwatosha ngamia wake wote. 21Pasipo kusema neno, yule mtumishi akamtazama kwa makini aone kama Bwana ameifanikisha safari yake, au la. 22Ikawa ngamia walipokwisha kunywa wote, yule mtumishi akampa huyo msichana pete ya puani ya dhahabu yenye uzito wa beka moja* na bangili mbili za dhahabu zenye uzito wa shekeli kumi.* 23Kisha akamuuliza, “Wewe ni binti wa nani? Tafadhali uniambie, je, kuna nafasi katika nyumba ya baba yako tutakapoweza kulala?” 24Yule msichana akamjibu, “Mimi ni binti wa Bethueli, mwana wa Milka aliyemzalia Nahori.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.