Mwanzo 23:15
Genesis 23:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nisikilize, bwana wangu, thamani ya ardhi hiyo ni shekeli 400 za fedha,* lakini hiyo ni nini kati yako na mimi? Mzike maiti wako.”
Genesis 23:15 in English
Genesis 23:15 · Berean Standard Bible
“Listen to me, my lord. The land is worth four hundred shekels of silver,* but what is that between you and me? Bury your dead.”
Context
13akamwambia Efroni wale watu wakiwa wanasikia, “Tafadhali nisikilize. Nitakulipa fedha za hilo shamba. Kubali kuzipokea ili niweze kumzika maiti wangu.” 14Efroni akamjibu Abrahamu, 15“Nisikilize, bwana wangu, thamani ya ardhi hiyo ni shekeli 400 za fedha,* lakini hiyo ni nini kati yako na mimi? Mzike maiti wako.” 16Abrahamu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: Shekeli 400 za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara. 17Hivyo shamba la Efroni huko Makpela karibu na Mamre, yaani shamba pamoja na pango lililokuwamo, nayo miti yote iliyokuwamo ndani ya mipaka ya shamba hilo, vilikabidhiwa,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.