Native Bible

Genesis 21:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.”

Genesis 21:24 in English

Genesis 21:24 · Berean Standard Bible

And Abraham replied, “I swear it.”

Context

22Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Abrahamu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. 23Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.” 24Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.” 25Ndipo Abrahamu akalalamika kwa Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamekinyangʼanya. 26Lakini Abimeleki akasema, “Sijui ni nani ambaye amefanya hili. Hukuniambia, leo tu ndipo ninasikia habari zake.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.