Mwanzo 21:13
Genesis 21:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitamfanya huyu mwana wa mtumishi wako wa kike kuwa taifa pia, kwa sababu naye ni uzao wako.”
Genesis 21:13 in English
Genesis 21:13 · Berean Standard Bible
But I will also make a nation of the slave woman’s son, because he is your offspring.”
Context
11Jambo hili lilimhuzunisha sana Abrahamu kwa sababu lilimhusu mwanawe. 12Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana na mtumishi wako wa kike. Sikiliza lolote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaki. 13Nitamfanya huyu mwana wa mtumishi wako wa kike kuwa taifa pia, kwa sababu naye ni uzao wako.” 14Kesho yake asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari. Akaviweka mabegani mwa Hagari, akamwondoa pamoja na kijana. Hagari akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba. 15Maji yalipokwisha kwenye kiriba, akamwacha kijana chini ya mojawapo ya vichaka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.