Mwanzo 2:24
Genesis 2:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Genesis 2:24 in English
Genesis 2:24 · Berean Standard Bible
For this reason a man will leave his father and mother and be united to his wife, and they will become one flesh.*
Context
22Kisha Bwana Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume. 23Huyo mwanaume akasema,
“Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu
na nyama ya nyama yangu,
ataitwa ‘mwanamke,’*
kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.” 24Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. 25Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.