Native Bible

Genesis 19:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akamwambia, “Vema sana, nitalikubali hili ombi pia, sitauangamiza mji ulioutaja.

Genesis 19:21 in English

Genesis 19:21 · Berean Standard Bible

“Very well,” he answered, “I will grant this request as well, and will not demolish the town you indicate.

Context

19Mtumishi wenu amepata kibali mbele ya macho yenu, nanyi mmeonyesha wema mkubwa kwangu kwa kuokoa maisha yangu. Lakini siwezi kukimbilia milimani, janga hili litanikumba, nami nitakufa. 20Tazama, hapa kuna mji karibu wa kukimbilia, nao ni mdogo. Niruhusuni nikimbilie humo, ni mdogo sana, ama sivyo? Ndipo maisha yangu yatasalimika.” 21Akamwambia, “Vema sana, nitalikubali hili ombi pia, sitauangamiza mji ulioutaja. 22Lakini ukimbilie huko haraka, kwa sababu sitaweza kufanya lolote mpaka ufike huko.” (Ndiyo maana mji huo ukaitwa Soari.*) 23Wakati Loti alipofika Soari, jua lilikuwa limechomoza katika nchi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.