Native Bible

Genesis 17:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako.

Genesis 17:6 in English

Genesis 17:6 · Berean Standard Bible

I will make you exceedingly fruitful; I will make nations of you, and kings will descend from you.

Context

4“Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. 5Jina lako hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Abrahamu,* kwa maana nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi. 6Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako. 7Nitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako. 8Nchi yote ya Kanaani, unakoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na uzao wako, nami nitakuwa Mungu wao.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.