Mwanzo 14:19
Genesis 14:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye akambariki Abramu, akisema, “Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na nchi.
Genesis 14:19 in English
Genesis 14:19 · Berean Standard Bible
and he blessed Abram and said: “Blessed be Abram by God Most High, Creator of heaven and earth,
Context
17Abramu aliporudi baada ya kumshinda Mfalme Kedorlaoma na wale wafalme waliojiunga naye, mfalme wa Sodoma akatoka kwenda kumlaki katika Bonde la Shawe (yaani Bonde la Mfalme). 18Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu alipoleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. 19Naye akambariki Abramu, akisema,
“Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana,
Muumba wa mbingu na nchi. 20Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana,
ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako.”
Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu. 21Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu na hizo mali uchukue wewe mwenyewe.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.