Mwanzo 1:6
Genesis 1:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.”
Genesis 1:6 in English
Genesis 1:6 · Berean Standard Bible
And God said, “Let there be an expanse * between the waters, to separate the waters from the waters.”
Context
4Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. 5Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza. 6Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.” 7Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo. 8Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.