Native Bible

Genesis 1:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mungu akafanya mianga miwili mikubwa: mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota.

Genesis 1:16 in English

Genesis 1:16 · Berean Standard Bible

God made two great lights: the greater light to rule the day and the lesser light to rule the night. And He made the stars as well.

Context

14Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbalimbali, siku na miaka, 15nayo iwe mianga kwenye nafasi ya anga ya kutia nuru juu ya dunia.” Ikawa hivyo. 16Mungu akafanya mianga miwili mikubwa: mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota. 17Mungu akaiweka katika nafasi ya anga iangaze dunia, 18itawale usiku na mchana, na ikatenganishe nuru na giza. Mungu akaona kuwa hili ni jema.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.