Native Bible

Galatians 6:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Angalieni herufi kubwa nitumiazo ninapowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe!

Galatians 6:11 in English

Galatians 6:11 · Berean Standard Bible

See what large letters I am using to write to you with my own hand!

Context

9Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa. 10Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio. 11Angalieni herufi kubwa nitumiazo ninapowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe! 12Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili wanataka wawalazimishe kutahiriwa. Sababu pekee ya kufanya hivyo ni kuepuka kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo. 13Hata wale waliotahiriwa wenyewe hawaitii sheria, lakini wanataka ninyi mtahiriwe ili wapate kujivuna kwa habari ya miili yenu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.