Wagalatia 6:10
Galatians 6:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio.
Galatians 6:10 in English
Galatians 6:10 · Berean Standard Bible
Therefore, as we have opportunity, let us do good to everyone, and especially to the family of faith.
Context
8Apandaye kwa mwili, katika mwili wake atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. 9Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa. 10Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio. 11Angalieni herufi kubwa nitumiazo ninapowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe! 12Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili wanataka wawalazimishe kutahiriwa. Sababu pekee ya kufanya hivyo ni kuepuka kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.