Wagalatia 5:3
Galatians 5:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote.
Galatians 5:3 in English
Galatians 5:3 · Berean Standard Bible
Again I testify to every man who gets himself circumcised that he is obligated to obey the whole law.
Context
1Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa. 2Sikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba kama mkikubali kutahiriwa, basi Kristo hatawafaidia chochote. 3Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote. 4Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu. 5Kwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.