Native Bible

Galatians 4:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ile hali ya furaha mliyokuwa nayo imekwenda wapi? Naweza kushuhudia kwamba, kama ingewezekana mngengʼoa macho yenu na kunipa mimi.

Galatians 4:15 in English

Galatians 4:15 · Berean Standard Bible

What then has become of your blessing? For I can testify that, if it were possible, you would have torn out your eyes and given them to me.

Context

13Ninyi mwajua kwamba ni kwa ajili ya udhaifu wangu niliwahubiria Injili. 14Ingawa hali yangu iliwatia majaribuni, hamkunidharau wala kunidhihaki, bali mlinikaribisha kama malaika wa Mungu, kama vile Kristo Yesu. 15Ile hali ya furaha mliyokuwa nayo imekwenda wapi? Naweza kushuhudia kwamba, kama ingewezekana mngengʼoa macho yenu na kunipa mimi. 16Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa kuwaambia kweli? 17Hao wana shauku ya kuwapata lakini si kwa kusudi zuri. Wanachotaka ni kuwatenga mbali nasi, ili ninyi mpate kuwaonea wao shauku.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.