Native Bible

Galatians 1:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote,

Galatians 1:16 in English

Galatians 1:16 · Berean Standard Bible

to reveal His Son in me so that I might preach Him among the Gentiles, I did not rush to consult with flesh and blood,

Context

14Nami niliendelea sana katika dini ya Kiyahudi kuliko Wayahudi wengi wa rika yangu maana nilijitahidi sana katika desturi za baba zangu. 15Lakini ilipompendeza Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu na kuniita kwa neema yake, 16alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote, 17wala sikupanda kwenda Yerusalemu kuwaona hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda mara moja Arabuni na kisha nikarudi Dameski. 18Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kuonana na Kefa* na nilikaa naye siku kumi na tano.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.