Native Bible

Ezekiel 7:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kila mkono utalegea na kila goti litakuwa dhaifu kama maji.

Ezekiel 7:17 in English

Ezekiel 7:17 · Berean Standard Bible

Every hand will go limp, and every knee will turn to water.

Context

15“Nje ni upanga, ndani ni tauni na njaa, wale walioko shambani watakufa kwa upanga, nao wale waliomo mjini njaa na tauni vitawala. 16Wale wote watakaopona na kutoroka watakuwa milimani, wakiomboleza kama hua wa mabondeni, kila mmoja kwa sababu ya dhambi zake. 17Kila mkono utalegea na kila goti litakuwa dhaifu kama maji. 18Watavaa nguo ya gunia na kufunikwa na hofu. Nyuso zao zitafunikwa na aibu na nywele za vichwa vyao zitanyolewa. 19Watatupa fedha yao barabarani, nayo dhahabu yao itakuwa najisi. Fedha yao na dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Bwana. Hawatashibisha njaa yao au kujaza matumbo yao kwa hiyo fedha wala dhahabu, kwa sababu imewaponza wajikwae dhambini.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.