Ezekieli 5:3
Ezekiel 5:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini chukua nywele chache uzifungie ndani ya pindo la vazi lako.
Ezekiel 5:3 in English
Ezekiel 5:3 · Berean Standard Bible
But you are to take a few strands of hair and secure them in the folds of your garment.
Context
1“Mwanadamu, sasa chukua upanga mkali na uutumie kama wembe wa kinyozi ili kunyolea nywele za kichwa chako na ndevu zako. Kisha uchukue mizani ya kupimia ukazigawanye nywele hizo. 2Wakati siku zako za kuzingirwa zitakapokwisha, choma theluthi moja ya hizo nywele zako kwa moto ndani ya mji. Chukua theluthi nyingine ya hizo nywele uzipige kwa upanga kuuzunguka mji wote na theluthi nyingine ya mwisho utaitawanya kwa upepo. Kwa kuwa nitawafuatia kwa upanga uliofutwa. 3Lakini chukua nywele chache uzifungie ndani ya pindo la vazi lako. 4Tena chukua nywele nyingine chache uzitupe motoni uziteketeze. Moto utaenea kutoka humo na kufika katika nyumba yote ya Israeli. 5“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Huu ndio Yerusalemu ambao nimeuweka katikati ya mataifa ukiwa umezungukwa na nchi pande zote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.