Ezekieli 48:17
Ezekiel 48:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sehemu ya malisho kwa ajili ya mji itakuwa na eneo la dhiraa 250* upande wa kaskazini, dhiraa 250 upande wa kusini, dhiraa 250 upande wa mashariki na dhiraa 250 upande wa magharibi.
Ezekiel 48:17 in English
Ezekiel 48:17 · Berean Standard Bible
The pastureland of the city will extend 250 cubits * to the north, 250 cubits to the south, 250 cubits to the east, and 250 cubits to the west.
Context
15“Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa 5,000* na urefu wa dhiraa 25,000, litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na malisho. Mji utakuwa katikati yake 16nao utakuwa na vipimo hivi: upande wa kaskazini dhiraa 4,500,* upande wa kusini dhiraa 4,500, upande wa mashariki dhiraa 4,500 na upande wa magharibi dhiraa 4,500. 17Sehemu ya malisho kwa ajili ya mji itakuwa na eneo la dhiraa 250* upande wa kaskazini, dhiraa 250 upande wa kusini, dhiraa 250 upande wa mashariki na dhiraa 250 upande wa magharibi. 18Eneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa 10,000 upande wa mashariki na dhiraa 10,000 upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula. 19Watumishi wa mji wanaolima shamba hili watatoka katika makabila yote ya Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.