Native Bible

Ezekiel 48:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa 5,000* na urefu wa dhiraa 25,000, litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na malisho. Mji utakuwa katikati yake

Ezekiel 48:15 in English

Ezekiel 48:15 · Berean Standard Bible

The remaining area, 5,000 cubits * wide and 25,000 cubits long, will be for common use by the city, for houses, and for pastureland. The city will be in the center of it

Context

13“Kando ya nchi ya makuhani, Walawi watakuwa na mgawo wa urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. Urefu wake utakuwa jumla dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. 14Hawataruhusiwa kuuza wala kuibadilisha hata mojawapo. Hii ndiyo sehemu nzuri ya nchi kuliko nyingine zote, hivyo haitakuwa mikononi mwa watu wengine, kwa sababu ni takatifu kwa Bwana. 15“Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa 5,000* na urefu wa dhiraa 25,000, litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na malisho. Mji utakuwa katikati yake 16nao utakuwa na vipimo hivi: upande wa kaskazini dhiraa 4,500,* upande wa kusini dhiraa 4,500, upande wa mashariki dhiraa 4,500 na upande wa magharibi dhiraa 4,500. 17Sehemu ya malisho kwa ajili ya mji itakuwa na eneo la dhiraa 250* upande wa kaskazini, dhiraa 250 upande wa kusini, dhiraa 250 upande wa mashariki na dhiraa 250 upande wa magharibi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.