Ezekieli 48:16
Ezekiel 48:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
nao utakuwa na vipimo hivi: upande wa kaskazini dhiraa 4,500,* upande wa kusini dhiraa 4,500, upande wa mashariki dhiraa 4,500 na upande wa magharibi dhiraa 4,500.
Ezekiel 48:16 in English
Ezekiel 48:16 · Berean Standard Bible
and will have these measurements: 4,500 cubits * on the north side, 4,500 cubits on the south side, 4,500 cubits on the east side, and 4,500 cubits on the west side.
Context
14Hawataruhusiwa kuuza wala kuibadilisha hata mojawapo. Hii ndiyo sehemu nzuri ya nchi kuliko nyingine zote, hivyo haitakuwa mikononi mwa watu wengine, kwa sababu ni takatifu kwa Bwana. 15“Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa 5,000* na urefu wa dhiraa 25,000, litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na malisho. Mji utakuwa katikati yake 16nao utakuwa na vipimo hivi: upande wa kaskazini dhiraa 4,500,* upande wa kusini dhiraa 4,500, upande wa mashariki dhiraa 4,500 na upande wa magharibi dhiraa 4,500. 17Sehemu ya malisho kwa ajili ya mji itakuwa na eneo la dhiraa 250* upande wa kaskazini, dhiraa 250 upande wa kusini, dhiraa 250 upande wa mashariki na dhiraa 250 upande wa magharibi. 18Eneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa 10,000 upande wa mashariki na dhiraa 10,000 upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.