Ezekieli 47:21
Ezekiel 47:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mtagawanya nchi hii miongoni mwenu kufuatana na makabila ya Israeli.
Ezekiel 47:21 in English
Ezekiel 47:21 · Berean Standard Bible
You are to divide this land among yourselves according to the tribes of Israel.
Context
19Upande wa kusini utaanzia Tamari hadi kufikia maji ya Meriba-Kadeshi, kisha utaambaa na Kijito cha Misri hadi Bahari Kuu. Huu utakuwa ndio mpaka wa kusini. 20Upande wa magharibi, Bahari Kuu itakuwa ndio mpaka hadi kwenye sehemu mkabala na Lebo-Hamathi. Huu utakuwa ndio mpaka wa magharibi. 21“Mtagawanya nchi hii miongoni mwenu kufuatana na makabila ya Israeli. 22Mtaigawanya kuwa urithi kwa ajili yenu na kwa ajili ya wageni wanaoishi miongoni mwenu na ambao wana watoto. Wao watakuwa kwenu kama wenyeji wazawa wa Israeli, pamoja na ninyi watagawiwa urithi miongoni mwa makabila ya Israeli. 23Katika kabila lolote mgeni atakapoishi hapo ndipo mtakapompatia urithi wake,” asema Bwana Mwenyezi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.