Ezekieli 4:12
Ezekiel 4:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nawe utakula chakula kama vile ambavyo ungekula mkate wa shayiri, uoke mkate mbele ya macho ya watu, ukitumia kinyesi cha mwanadamu.”
Ezekiel 4:12 in English
Ezekiel 4:12 · Berean Standard Bible
And you shall eat the food as you would a barley cake, after you bake it over dried human excrement in the sight of the people.”
Context
10Pima shekeli ishirini* za chakula utakachokula kwa kila siku, nawe utakula kwa wakati uliopangwa. 11Pia pima maji moja ya sita ya hini,* nawe utakunywa kwa wakati uliopangwa. 12Nawe utakula chakula kama vile ambavyo ungekula mkate wa shayiri, uoke mkate mbele ya macho ya watu, ukitumia kinyesi cha mwanadamu.” 13Bwana akasema, “Hivi ndivyo watu wa Israeli watakavyokula chakula kilicho najisi miongoni mwa mataifa ninakowapeleka.” 14Ndipo nikasema, “Sivyo Bwana Mwenyezi! Kamwe mimi sijajitia unajisi. Tangu ujana wangu hadi sasa sijala kamwe kitu chochote kilichokufa au kilichoraruliwa na wanyama wa mwituni. Hakuna nyama yeyote najisi iliyoingia kinywani mwangu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.