Ezekieli 39:16
Ezekiel 39:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
(Pia mji uitwao Hamona* utakuwa humo.) Hivyo ndivyo watakavyoisafisha nchi.’
Ezekiel 39:16 in English
Ezekiel 39:16 · Berean Standard Bible
(Even the city will be named Hamonah.*) And so they will cleanse the land.
Context
14“ ‘Watu wataajiriwa mara kwa mara kuisafisha nchi. Baadhi yao watapita nchini kote na zaidi yao hao wengine, watawazika wale waliosalia juu ya uso wa nchi. Mwisho wa hiyo miezi saba wataanza upekuzi wao. 15Wakati wanapopita nchini kote na mmoja wao akaona mfupa wa mwanadamu, ataweka alama kando yake mpaka wachimba kaburi wawe wameuzika katika Bonde la Hamon-Gogu. 16(Pia mji uitwao Hamona* utakuwa humo.) Hivyo ndivyo watakavyoisafisha nchi.’ 17“Mwanadamu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ita kila aina ya ndege na wanyama wote wa mwituni, waambie: ‘Kusanyikeni mje pamoja kutoka pande zote kwa ajili ya dhabihu ninayowaandalia, dhabihu kuu katika milima ya Israeli. Huko mtakula nyama na kunywa damu. 18Mtakula nyama za watu mashujaa na kunywa damu za wakuu wa dunia kana kwamba ni za kondoo dume na kondoo wake, mbuzi na mafahali, wote walionona kutoka Bashani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.