Ezekieli 31:3
Ezekiel 31:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Angalia Ashuru, wakati fulani ilikuwa mwerezi huko Lebanoni, ukiwa na matawi mazuri ukitia msitu kivuli; ulikuwa mrefu sana, kilele chake kilipita majani ya miti yote.
Ezekiel 31:3 in English
Ezekiel 31:3 · Berean Standard Bible
Look at Assyria, a cedar in Lebanon, with beautiful branches that shaded the forest. It towered on high; its top was among the clouds.
Context
1Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza, neno la Bwana likanijia, kusema: 2“Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na makundi yake ya wajeuri:
“ ‘Je, ni nani awezaye kulinganishwa
na wewe katika fahari. 3Angalia Ashuru, wakati fulani ilikuwa mwerezi huko Lebanoni,
ukiwa na matawi mazuri ukitia msitu kivuli;
ulikuwa mrefu sana,
kilele chake kilipita majani ya miti yote. 4Maji mengi yaliustawisha,
chemchemi zenye maji mengi ziliufanya urefuke;
vijito vyake vilitiririka pale
ulipoota pande zote
na kupeleka mifereji yake
kwenye miti yote ya shambani. 5Hivyo ukarefuka
kupita miti yote ya shambani;
vitawi vyake viliongezeka
na matawi yake yakawa marefu,
yakitanda kwa sababu ya wingi wa maji.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.